Tuesday, November 13, 2012

Gomesa Tv

Buibui apata msaada Tanzania Music Power


TANZANIA MUSIC P0WER ni Jumuia mpya ya kiharakati iliyoingia rasmi katika kuokoa kizazi cha mziki wa bongo fleva Tanzania,kwamara ya kwanza imeingia makubaliano na msanii wa bongo fleva Frenk Lewis Katende Kivunike anayefahamika kwa jina la BUIBUI. TMP imeingia makubaliano na Buibui baada ya kukiona kipaji chake na juhudi zake katika kufanya kazi ya muziki wa kizazi kipya. TANZANIA MUSIC POWER inatambua uwepo wa vyombo vya habari na mchango wao katika tasnia ya muziki,hivyo inawaomba wasanii, wanahabari na wadau wote wa muziki kusaidia katika kuwainua wasanii ambao wamechangia kuuweka muziki wa Tanzania ulipo sasa.

Historia ya Buibui ni ndefu sana toka alipo zaliwa mpaka sasa na muda si mrefu TANZANIA MUSIC POWER itatoa kitabu cha maisha ya BUIBUI kuanzia watu aliowahi kushirikiana nao na mpaka kudondoka katika tasnia ya muziki.

BUIBUI amerudi sasa na T.M.P inatarajia kutambulisha wimbo wake mpya ambao utaanza kurushwa hewani rasmi baada ya kumalizika kwa makubaliano ya mwisho na TMP.

Hivyo basi tunapenda kuchukua nafasi hii kuomba watanzania wote kumpokea BUIBUI,tunatanguliza shukrani za dhati kwa watanzania wote.
ahsanteni sana.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi