Thursday, November 15, 2012

Gomesa Tv

Barnaba kuhamisisha ujenzi wa Hosteri 30


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Barnaba ameungana na mabalozi wengine katika kuhamasisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana. Barnaba anaunga na Nancy Sumari, Faraja Kota na Rebeka Giuni katika kampeni hiyo inayolenga kukusanya bilioni 2.3 na kujenga hosteli 30 ambapo Barnaba atashiriki matembezi hayo.
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeandaa matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 30 ya wanafunzi wa kike.
Matembezi hayo yataanzia katika eneo la Mlimani City kesho kuanzia saa moja hadi saa tano asubihi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mary Nagu. Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa alisema kuwa matembezi hayo ni moja kati ya harakati ya kuchangisha bilioni 2.3 kwa ajaili ya ujenzi wa mabweni hayo yatakayohudumia wanafunzi wa kike 1,504.
Alisema kuwa mikoa ambayo inahitaji mabweni hayo kwa wingi ni Mara, Kigoma, Rukwa, Tanga, Dodoma,Manyara, Lindi na Magu .

Alisema kuwa ni vema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za ujenzi wa mabweni hayo kwa kununua fomu za ushiriki ambapo alisema kuwa fomu zinauzwa kwa shilingi 20000/= katika ofisi za TEA.“ Mimi naona kuwa hizi ni juhudi nzuri ambazo zinafanywa na hawa watu wa TEA kwa kushirikiana na mabalozi wetu mbalimbali  na kuna jukumu la kila mmoja wetu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hawa wanasaidiwa uhakika wao wa mahala pa kulala kwa kuwajengea hizi hosteli” alisema Waziri Kawambwa.

Lengo la serikali ni kujenga mabweni 100 kwa lengo la kuhudumia wanafunzi wa kike 4,800 nchini ili kuwanusuru na hatari ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi