Tuesday, October 23, 2012

Gomesa Tv

Wasanii wavaa vibaya kukiona

Katibu Mtendaji wa shirikisho la filamu Tanzania 'TAFF, amesema hivi sasa wamuamua kuwa wakali na kutaka kutoa tamko kwa wasanii wote wa filamu nchini, kulinda maadili kuanzia kwenye maisha.....
yao ya kila siku wanapokuwa majukwaani na kwenye filamu zao.
Alisema wamepewa mamlaka na Seriakli ya kudhibiti hali hiyo baada ya kuzagaa picha chafu za waigizaji wa filamu nchini Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, kati tamasha la Serengeti Fiesta2012.

Aidha alisema kwamba walikuwa wakitaka kutoa tamko juu ya wasanii hao, lakini waliwahi kuomba radhi jambo ambalo liliwafanya wasitishe na kuandaa tamko kwaajili ya wasanii wote wenye tabia kama hizo.

Alisema pia katika filamu ambazo mara nyingi nazo zimekuwa hazina maadili watakuwa wakizifuatilia moja baada ya nyingine, baada ya kuona kamati ya maadili iliyopo kwenye Bodi ya Filamu kushindwa kufanya kazi zake na kupelekea filamu nyingi kuingia sokoni zikiwa na maovu kibao.
(Raisi wa TAFU Simon Mwakfwamba, na katibu mtendaji William Makubi)

Makubi alisema kwamba sasa hivi watakuwa makini kwani watakuwa wakiangalia kosa gani msanii kifanya, kisha wanatoa Onyo, au kuzuia kazi na ikizidi basi wanamfungia msanii huyo kutoigiza tena.
Pia liongezea kwa kusema hata maproducer  ambao wamekuwa wakiongoza fialmua mabzo baadae zinakuja kuwa na tatizo katika maadili nao wataingizwa kwenye mkumbo huo.

Alisema miongoni mwa vitu ambavyo watakuwa wakiangalia ni Mavazi na Lugha, katika filamu zote.
Pia alikiri kwamba kwa sasa wanamapungufu makubwa na ndiyo maana kazi inatoka mpaka inasambaa kwa kila mtu na kama maadili yanakuwa tayari yameshapotoka wao ndiyo wanakuja kupata habari wakiwa tayari wamesha chelewa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi