Wednesday, October 17, 2012

Gomesa Tv

Wasanii wajitokeza kujiunga na NSSF

Leo wasanii wa filamu nchini walikusanyika pamoja katika semina maalum ambayo ilikuwa ikitolewa na Shirika la Hifadhi ya mfuko wa kijamii la NSSF. Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni hiyo Crescentius Magori, alisema shirika hilo limeamua kufanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi wakiwemo wasanii ambao hawajaajiliwa wamekuwa wakikosa fulsa ya kujiunga na mfuko huo. Alisema mara nyingi watu walioajiliwa ndiyo wamekuwa na nafasi kubwa ya kupata huduma zitolewazo na mfuko huo ikiwemo huduma ya matibabu, kiinua mgongo na huduma zingine ambazo zinatokana wanachama wa mfuko huo. Aidha alisema lengo la mfuko huo waajiliwa na wasiokuwa waajiliwa kuweza kupata huduma hiyo, lakini mwamko umekuwa mdogo sana kwa watu waliojiajili.
(Jacob Stephan 'J.B' akipata kitambulisho chake)


 Amesema kwakuwa hilo sio lengo lao ndiyo maana wameamua kutoa elimu kwa kila mtu hususani
Wasanii ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu na kuingiza kipato kingi ambacho humaliza kwa muda mfupi, na baadaye wanapopata matatizo hakuna wa kuwasaidia. Alitoa mfano kwa msanii Sajuki, Mzee Small na Vengu, ambao wanendelea kutabika kwa kusoma huduma mzuri. Alisema kama wangekuwa wamejiunga na mfuko huo, hivi sasa wangekuwa wanalipwa huku wakiendelea kupata huduma katika hospitali wanazotaka.

(Mkurugenzi muendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, akitoa kitambulisho kwa msanii Libert Msuya)        
(Raisi wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba, akitoa maelezo juu ya NSSF)
 Mr Magori alisema pia mwachama atakuwa na uwezo wa kukopa nyumba za NSSF, huku akilipa kidogokidogo kwa takriban mika 15, pia atakuwa na nafasi ya kukopa katika SACOSS ambazo zitaanzishwa na wasanii wenyewe lakini fedha zikitoka NSSF
 Big naye akiwa mmoja wa wasanii waliojiunga na mfuko huo
 Deugratus
Maya

Rechol naye alikuwepo

Steve Nyerere naye alikuwa mmoja waliopokea vitambulisho


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi