Wednesday, October 31, 2012

Gomesa Tv

Suma lee aibiwa gari na kusekwa polisi

Baada ya mwanamuziki Seif Shambani ‘Matonya’ kuibiwa vitu vyake vya ndani, na baadaye Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ kuibiwa Power window ya gari lake aina ya Verrosa..
sasa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Ismail Thabiti ‘Suma lee’ ameibiwa gari lake aina ya Land Cruiser  T 504 BRF, maeneo ya Coco Beach ambapo alikuwa ameliegesha.

Suma Lee aliongea na Bongo Unit, na kusema kwamba aliliegesha gari lake maeneo ya Coco Beach, na baadaye kwenda kuzunguka kidogo maeneo hayo, lakini baadaye aliporudi gari hilo hakuliona.
Alisema baada ya hapo alimfuata mlizni aliyekuwa maeneo hayo,ambapo wakati anakuja kuliegesha alimuona, hivyo akaanza kumuuliza jambo ambalo lilimpelekea kushikwa na hasira na kupishana naye maneno.
Alizidi kufunguka na kusema kwamba  baada ya hapo, akaja muhusika wa hapo na kumchukua na kumpeleka kwenye kituo cha polisi cha Ostabai.
“Lakini polisi sikukaa nikatoka na kufungua Rb katika kituo cha hapo hapo Ostabei Polisi” alisema.
Alisema namba aliyofungulia ni OB/RB/19237/2012, ambayo itamwezesha kumtafuta mtuhumiwa wake popote na kumfungulia mashitaka.


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi