Saturday, October 6, 2012

Gomesa Tv

Rick Ross aleta vituko Dar

 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross ameshindwa kuonana na waandishi wa Habari katika hoteli ambapo alitakiwa kuongea naye kisa nguo zake bado hazijafika kutoka nchini Marekani. Mwanamuziki huyoalisema begi lake bado halijafika, jambo ambalo liliwafanya waandaaji wa tamasha hilo....
kuanza kuingia mitaani kuchukua nguo ili kuja kulinganisha naye kama zinaweza kumtoa chicha na kuingia hotelini kwaajili ya mahojiano hayo. Hata hivyo zililetwa nguo za kila aina lakini cha ajabu nguo hizo zilishindwa kumuonea, jambo ambalo lilizidi kumweka katika hali ya utata na kusema si shuki ndani ya gari, mpaka zije nguo zangu. Walipoona haitoshi, ikabidi wakamshonee nguo mbili, kwa hiyo mwanamuziki huyo anasubiri nguo za kushonesha ili aweze kufanya nazo mahojiano baada zile spesho kushindikana. hata hivyo waandishi walisema anaweza kuingia hata tumbo wazi, kwakuwa video zake nyingi yupo tumbo wazi, ili wapate kuziona tatooo zake.


Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Allan Chonjo akisalimiana na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross mara baada ya kuwasili usiku huu ndani ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere!

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi