Wednesday, October 3, 2012

Gomesa Tv

Mr India na Meneja wake waigawanya Poteza Record

Studio ya kurekodi muziki ambayo ilikuwa ikiibuka kwa kasi chini ya Producer Suresh au Mr India na kumtoa Dogo Aslay na Bibi Cheka, imegawanyika vipande viwili, kutokana na kutoelewana kwake na mkurugenzi wa Studio hiyo Saidi Fella pamoja na meneja wa studio Yusufu Chambuzo, kutokana na kile kinachodaiwa kwamba Producer huyo...........
                                    (Studio mpya ya Saidi Fella)                            
    aligoma kwenda makao mapya ya wasanii wa Mkubwa na wanawe ambao ndiyo wenye studio hiyo. Chambuso alisema kwamba baada ya kuhama sehemu ambayo walikuwa wakifanyia mazoezi zamani, ilibidi pia wahamishe studio hiyo na kuelekea makazi mapya lakini ndipo producer huyo alipogoma na kusema hawezi kwenda popote. Meneja aliendelea kusema kwamba ikabidi kama hataki kuondoka basi wachukue vitu vyao, kwakuwa tayari walishapata Producer mwingine, ambaye pia ni mwimbaji Awadhi Salim 'Shirko'.

     


Baada ya kuambiwa hivyo, producer huyo alikataa ndipo meneja na Saidi Fella waliamua kutaka kuchukuwa vitu vyao vya muziki, lakini producer Suresh, inasadikiwa aliwaomba ili wamwachie vifaa hivyo kwakuwa ndiyo sehemu ya maisha yake. Meneja anasema kwakuwa hawakuwa na ubaya naye, wala tatizo ikabidi wamwachie na wao kununua vifaa nipya ambavyo hadi sasa wameshakamilisha na kuanza kazi kama zamani.
Hivi sasa studio hiyo inaitwa Vibe Record ikiwa chini ya Producer Shirko, ambaye ni raia wa Kenya aliamua kuja kufanya kazi ya muziki Tanzania, na ndiye aliyetengeneza wimbo wa Mi na wewe pia kuchana katika wimbo huo wa  Two Berry (Berry Black na Berry White)


Shirko

Shirko

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi