Wednesday, October 31, 2012

Gomesa Tv

Kasheshe la Diamond, Pasha na H baba juu ya wimbo mpya

Nyota wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz', anashutumiwa na mwanamuziki Hamisi Ramadhani 'H. Baba' wimbo wake mpya ambao ameutoa hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Nataka kulewa.

H Baba alieleza kwamba siku hiyo Diamond aliingia KGT, na kumkuta yeye na Abubakari Katwira 'Q Chilla' akiingiza chorus katika wimbo huo,  ndipo akavutiwa nao akaanza kuumba huku akicheza akionyesha jinsi gani alivyovutiwa na wimbo huo.
Anazidikusisitiza na kusema baada ya mwanamuziki huyo kuondoka wao waliendelea na kuingiza voko zingine, na baada ya hapo waliondioka.
Lakini anasema mara ghafla anasikia mwanamuziki huyo ametoa wimbompya ambao unakwenda kwa jina la Nataka kulewa, wakati yeye tayari alikuwa na wimbokama huo.
H baba
Pasha

H Baba nasema baada ya kuendelea kufuatilia ndipo akagundua hata merodi aliyotumia mwanamuziki huyo ni ile ya kwake, lakini ndipo mara akasikia pasha naye akilalamika kwamba na yeye ameibiwa baadhi ya staili katika wimbo huo mpya na baadhi ya manjonjo.
H Baba anasema wimbo huo ambao tarehe ambayo aliingiza voko na biti ipo, lakini chaajabu Vocol kwa sasa hazionekani,lakini biti ipo kama kawaida.

Alisema tukio hilo linamshangaza sana, lakini kwake hajali kwakuwa anaflash ambayo aliingiza Demo hiyo ambayo kwake ni kama ushahidi.  Hata hivyo amesema hatochukuwa maamuzi yoyote mpaka mwanamuziki huyo atakapojibu tuhuma hizo kama atakubali au kukataa, na ndipo atakapoangalia njia ya kuchukuwa.
 

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi