Tuesday, October 23, 2012

Gomesa Tv

Dotnata apata baraka Nigeria za kufungua kanisa

Mwigizaji na mfanyabiasha na aliyewahi kuwa mwanamuziki Dotnata Poshi, amesema kwa sasa ameaokoka kabisa na kuamua kufungua kanisa kubwa lengo likiwa kuwashawishi wasanii wenzake kuachana na  maasi na hatmaye kumrudia mungu....

Dotnata ambaye alianza kwa kufafanua jina lake alisema watu wengi wamezoea kumwamwita jina hilo bila kujua msingi wake, kwamba yeye jina lake ni Doto na ameunganisha na jina lake la ubatizo Illuminate ambapo akachukuwa jina la kwanza la Dot na kuunganisha jina la mwisho na  nate na kupata Dotnata.

(Mchungaji Joshua wa Nigeria)
Alisema aliamua kwenda Nigeria  kwa mchungaji Joshua ambaye ni maarufu sana Afrika na Dunia nzima na kuwavutia vigogo mbalimbali wa Seriakali za Afrika, ili kwenda kuchukuwa baraka akwaajili ya kuanzisha kanisa hilo.

Alisema baada ya kurudi huko na kupata baraka hizo za kufungua kanisa hivi sasa anasomea masomo ya Biblia ili baadaye kuja kuwa  mchungaji,ingawa kwa sasa yupo kama mama wa kanisa. Aidha alidai kwa sasa kanisa lake litakuwa na wahubiri kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kufanya sehemu hiyo kuwa takatifu, na baada ya hapo ataanza kutoa elimu kwa wasanii waweze kuokoka ili kumrudia mungu.

Alisema kwa sasa hawezi kumlaumu, msanii ambaye anafanya mambo ya ajabu ajabu kwakuwa anaamini ni ujana unamsumbua na  ukifika muda atabadirika. Dotnata alizidi kusisitiza kwa kusema katika kanisa lake anategemea pia kumchukua msanii Ray C, ambaye naye ameokoka na baadaye kumuunganisha kwenye kanisa hilo pamoja na mwanamuziki Asha Madinda ambaye naye ameokoka na kuwachukuwa kwenye kanisa lake.

Mwisho alimalizia kwa kusema kanisa hilokwa hivi sasa lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili, ingwa pia limeruhusiwa kuendelea na kazi zake za ibada.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi