Saturday, October 20, 2012

Gomesa Tv

Batuli kufuta machozi ya Watanzania

 Nyota wa filamu hapa nchini ambaye nyota yake yazidi kushika kasi kila kukicha kutokana na hisia kali anazozionyesha kwenye filamu yake, amesema kamwe hawezi kujidhalilisha kwaajili ya kutafuta umaarufu, ila anategeema kufanya filamu zaidi za kijamii ili kuweza kumjengea jina na heshima kwa jamii inayomzunguka. Batuli aliongeza kwa kusema anaamini ni kazi ngumu sana  kwa watu kufikia kiwango cha marehemu Steven Kanumba, lakini kwa yeye anaamini atafikia huko kutokana na kujituma kwake.
 Anasema hawezi kukubaliana  kuona watu  wanaichafua Bongo Movie sababu ya wasanii wachache hususani wa  kike, kwakuwa ni huruka ya mtu, hivyo haiwezekani kuwachanga hata wasiokuwemo kwenye tabia hiyo. Batuli alizidi kusema kwamba kila lawama ya tabia mbaya  zinaangukia kwa wasanii wa Bongo Movie, na kuwapelekea  Watanzania kutokuwa na imani na filamu zao kutokana kuchukizwa na tabia , jambo ambalo anaamini amekuja kuibadilisha imani hiyo.
Pia alimalizia kwa kusema anachotaka zaidi na kuwaomba Watanzania waacha kufuatilia filamu za Mtu mmoja, na badala yake waangalia vipaji tofuati  kwani ndipo wanaweza kugundua filamu tofauti na kuzitenga kati ya nzuri na mbaya.Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi