Friday, September 28, 2012

Gomesa Tv

Twanga Pepeta kurudi Jijini

Wakali wa burudani Nchini, African Stars Band "Twanga Pepeta" wanaondoka leo Alhamisi (27-09-2012) kuelekea kanda ya ziwa kwa ziara ya maonyesho kwa siku tatu kuanzia kesho siku ya Ijumaa(28-09-2012) ambapo itakuwa Kahama katika ukumbi wa Club Dimpoz.
Siku ya Jumamosi watakuwa katika ukumbi wa Jocker's live pub uliopo katika maeneo ya Iloganzara Jijini Mwanza.
Twanga Pepeta watamalizia kufanya onyesho Geita katika ukumbi wa Desire na wanataraji kurejea Jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu (01-10-2012) na kuendelea na maonyesho yake kama kawaida.
Itapokuwa Mwanza Twanga Pepeta inataraji kumtambulisha Mwimbaji wao mpya Kalala Jr aliyejiunga na Twanga Pepeta hivi karibuni akitokea katika Bendi ya Mapacha watatu, Sambamba na kumtambulisha Mwimbaji huyo pia Twanga Pepeta itatambulisha wimbo wake mpya wa Nyumbani ni nyumbani ambao ni wimbo aliutunga mara tu baada ya kujiunga na Twanga Pepeta.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi