Tuesday, September 18, 2012

Gomesa Tv

Saraha na Fundi Samweli kurudi nchini kwao Sweden


MWANAMUZIKI  aliyekuwa akija kwa kasi katika muziki wa Bongo Fleva Saraha  amesema amebakiza siku chache za kuendelea kubaki nchini Tanzania, hivyo ameamua kwa sasa kuzimaliza kazi za wasanii wote na kuziachia ili aweze kuondoka  akiwa tayari amemaliza kazi zote.

Saraha ambaye yeye na Mumewe Fundi Samweli  ambaye pia ni producer mzuri, wote ni  raia wa Sweden, na waliishi hapa nchini kwa muda mrefu na kufanya kazi nyingi za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, zikiwemo zileza za N2N Solders, River Camp na nyingine nyingi . Hata hivyo alisema kwamba muziki wa Bongo Fleva watakuwa wakiufanya hata kama wakiwa nje ya Tanzania, kwakuwa umeshaingia ndani ya damu yao.
 

“Nitafanya muziki wa Bongo Fleva nchini Sweden kwa mtindo mwingine kabisa” alisema.
Pia mume wa mwanamuziki huyo, Fundi Samweri anayemiliki studio ya  Usanii  pia anatarajia (Soma zaidi)
kuondoka.
Amesema kwamba wakipata nafasi ya kuja, lakini sio kuja kuishi kama ilivyokuwa mwanzo, ila watakachokuwa wakifanya ni kuja kutembelea rafiki na baadaye kuondoka. Sara pia alisema ataendelea kushirikiana na baadhi ya wasanii kwa kuwatengenezea nyimbona kuwatumia, kupitia studio yao ya USANII.
Saraha akiwa na mumewe Fundi Samweli

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi