Thursday, September 27, 2012

Gomesa Tv

Mjue mwigizaji wa kike anayetikisa kwa sasa

 Katika kuibuka  kwa wasanii wapya wa kike na pia kupotea kwa baadhi yao leo hii blog yako ya BONGO UNIT, ambayo haina mbwembwe sana ila zaidi ni kukuletea utamu unaohusu wasanii wetu wa humu humu ndani, ili kuweza kuinua tasnia yetu. Leo hii nawaleteni msanii ambaye kwa sasa ndiye anayekuja kwa kasi na kuchukua nafasi za wasanii wengine ambao walikuwa wakivuma na sasa kupotea taratibu. Jina halisi ni Yobnesh Yusuph aambalo anapenda kulitumia kisanii ni Batuli . Mwigizaji huyu anasifa za urefu  ana mwili mnene kiasi, ngozi  wanasema maji ya kunde, mcheshi na asiyejua kukasirika hadi sasa ameshaigiza filamu zaidi ya tano  zilizotoka, ikiwemo Glory to Ramadhan ya Vicent Kigosi 'Ray' wa kampuni ya Rj , na ambazo ameigiza ila bado hazijaingia sokoni ni nyingi ikiwemo Long Time, Get Out za Stive Nyerere kutoka kampuni ya Nyerere The Power, Waves of Sorrow ya Vicent Kigosi, Fungate ya Cloud 112 katika kampuni yake ya CY & CY  na Cost To Cost ya Slim.  Hebu pata picha zake na uone kazi zake
 Angalia picha zake zaidi akiwa kwenye pozi


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi