Saturday, September 8, 2012

Gomesa Tv

(G.Habash-Times Fm-Maskani) HUKU (E. Kibonde -Clouds Fm-Jahazi) Saa 10 jioni

MUME  wa mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jay Dee' na mtangazaji maarufu aliyewahi kujipatia jina kutokana na utangazaji katika kipindi cha Jahazi kilichokuwa kikirushwa Clouds Fm hapa hapa nchini Tanzania Captain Gadner  Habash, jumatatu hii ya  Sept anatarajia kusikika kwa mara ya Kwanza katika stesheni ya Times Fm, akiendesha kipindi cha Maskani........... (Soma zaidi bonyeza Read More)


G. Habash amesema kipindi chake kitakuwa kikizungumzia masuala mbalimbali ya kijamii, maisha ya kila siku na vichekesho vya hapa na pale. Pia alisema katika kipindi hicho, atatumia jina la Captain kama kawaida kwakuwa jina hilo halikutokana na kipindi wala stesheni ambayo alikuwa akiitangaza mwanzo ila ni kutokana na uwezo wake wa kutangaza na kuwakabiri mashabiki wake.
Aidha alisema pia atahusisha baadhi ya matukio muhimu, kama habari za Michezo, magazeti, watu wakipiga stori  ndogo ndogo kutoka kwa waandishi wengine. Pia amesema kipindi chake, kitakuwa kikipiga stori kupitia Facebook, Twitte na mitandao mengine ya kijamiii, na kufanya kionekanane kama sehemu nyingine ya  kupigia stori kama vilena  ofisini, kijiweni na sehemu nyingine ambapo watu wanakutana.
Kutokana na maelezo hayo hivyo muda,  wakati na manjonjo yanafanana zaidi na kipindi cha Jahazi, ambacho kinaendeshwa na Anord Kayanda kwa sasa  huku kikibebwa umaarufu na swahiba wa karibu wa G . Habashi, Ephrahim Kibonde. Kazi itakuwa kwa mashabiki wa watangazaji haw wawili, kwani kila mmoja anachachu kwa mwenzake. Nani atahit, nani atapwaya kazi kwenu......

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi