Wednesday, September 12, 2012

Gomesa Tv

Madee ajibu tuhuma za Dogo Janja

 Baada ya mwanamuziki alitikisa katika kundi la Tip Top Connection, Abdul Laziz 'Dogo Janja' kulalamika kwenye Media mbalimbali kwamba ameombwa kutoa mashairi yaliyokuwa katika wimbo wa Anajua, aliomshirikisha Tunda Man Kiongozi wa kundi hilo Madee ameibuka na kusema kwamba jambo hilo si kweli.
Madee ambaye ndiyo kiongozi wa kundi hilo, na ndiye msanii wa kwanza kumtoa msanii Dogo Janja,alisema kwamba Dogo Janja anatapatapa hajui pa kushika na wala hawana mpango wa kumfuatilia.


Madee alisema kwa sasa wao wanaangaika katika nyimbo yao mpya ya Riziki, akiwa na wasanii wapya wa kundi akiwemo  Sungura, Desso, pamoja na TundaMan.
  Alisema wao wana nyimbo nyingi, na wala hawana mpango wa kumzuia asitumie wala kutoa mashaili ya wimbo huo. Pia amesema kwamba ameshatoa wasanii wengi kupitia kundi hilo, kwa hiyo hatoacha kusaidia wasanii wengine watakao hitaji msaada kutoka kwake kwakuwa hata yeye amesaidiwa hadikufika pale alipo sasa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi