Saturday, September 1, 2012

Gomesa Tv

Jenifer wa Kanumba, yamnyemelea ya Lulu.

 Nyota wa filamu za Bongo Movie,ambaye aliwika sana katika filamu za Steven Kanumba ya This is it na Uncle Jj Hanifa Daud anayejulikana zaidi kwa jina la Jenifer,  huenda yakamkuta kama yaliyomkuta Elizaberth Michael 'Lulu'. Hali hiyo imetokana na wazazi wa mwigizaji huyokusadikiwa kwamba mtoto wao wamemfanya mtaji wa kuvuna pesa. Baadhi ya wasanii walidai kwamba pindi ukimtaka msanii huyo, basi wazazi wake wanakaa kikao na fedha watakazo kutajia hapo huenda ukachanganyikiwa, jambo ambalo wanahisi wazazi hao kumfanya mtaji. Lakini hofu yao kwamba huenda mtoto huyo akazijua fedha mapema kutokana na kichwa anachopewa na wazazi wake kwamba anathamani kubwa kiasi hicho, na hatmaye kuja kuishi maisha ya tamaa na kuingia kwenye skendo za kila siku.
Jenifer akiwa na Kanumba
 Msanii mmoja alidai kwamba ukimtaka msanii huyo, basi unaweza kutajiwa milioni mbili au zaidi akiigiza kama Main Character, hali ambayo wanasema kwa umri wake ni mdogo sana ila wanafanya hivyo kama tamaa. Hali inaeleza zaidi kwamba pindi umri wake ukiinukia kiduchu kama wa lulu (7-18), huenda akatamani maisha ya kulipwa fedha nyingi kama wazazi wake wanavyompangia,hali ambayo itampelekea kujikuta akitumiwa vibaya na wenye fedha.
Wadau wa filamu wamewasihi wazazi wa mtoto huyo, kwamba aangalie zaidi masomo ya mtoto wao,na kama ataigiza basi aigie kama kipaji na sio wamfanye mtaji wa kuvunia pesa kwani hiyo inajijenga akili mwake na kuwa kama ya Lulu,aliyenza akiwa mdogo katika WAHAPAHAPA.....

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi