dotnata

dotnata
KARIBU KATIKA BURUDANI ZA WASANII WA FILAMU NA MUZIKI.... KUWA WA KWANZA!

Wednesday, May 15, 2013

Cloud 112 @ aja na filamu ya SHAHAADA kuipiku TOBA.


 Mwigizaji nyota wa filamu Issa Mussa 'Cloud 112' ameamua kuja na filamu kali, ambayo itakuja kuifunika filamu ya TOBA, ambayo hiyo itakuwa ikiitwa SHAHAADA. Katika filamu hiyo ambayo ameifanya hivi karibuni itakuwa na mahadhi ya kidini ya kiislamu na kuvutia watu wengi kutokana na matukio ya humo ndani
 Hebu pata baadhi ya picha ndani ya filamu hiyo ambayo inakuja kutikisa.






























Diamond Plutnum@ MP katika tamasha la nchini Congo

Diamond Plutnum anatarajia kupanda jukwaani na nguo za kijeshi za nchi ya Congo katika tamasha litakalo fanyika nchini humo , akiwa kama MP.

Mziki gani@ kuzinduliwa Dar Live


Mama Yeyooo " Nje ya Box ndani ya Live band Maisha Club



Saturday, May 11, 2013

Batuli alamikia karamu za waandishi.

Nyota wa filamu nchini, hivi karibuni baadhi ya magazeti yalimwandika kwamba anakansa ya titi na mwenyewe kukanusha kupitia Blog ya Bongo Unit, lakini leo hii ameandikwa tena kwenye moja ya Majarida na mwenyewe kujibu kama hivi:
 "Usipotoshe jamii kwa taaluma yako, mnanikwaza sana kwa habari isiyo ya kweli, tumieni kalamu zenu vizuri."

Huu ndiyo ushauri wa Dotnata kwa Jay Dee

Ushauri wangu kwa mdogo wangu Jide a.k.a cobra. Huu ni mtazamo wangu jamani
Nakushauri acha malumbano na kaka zako, shukuru mungu kwa hicho walichokusaidia
Ukumbuke ulikotoka.

Ebu mwimbie mungu wako aliyekupa sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni,  hivi hebu siku moja  wakusikie umemrudia mungu na bendi yako iendelee kutumbuiza nyimbo za mungu
Utapata mialiko mingapi? Utaokoa roho za watu wengi.

 Hakuna nyimbo zinazoongoza kwa mauzo kama nyimbo za mungu,  rudi kwa mungu wako. Nimesikia nyimbo yako juzi ya mwacheni mungu aitwe mungu. Ingawa si yote lakini ilinibariki,  Ukiona njia moja imebana ujue mungu Anakutafuta ufanye huduma yake. Ubarikiwe.

Steve Nyerere ageuka nyoka ndani ya Snake Kingdom

 Hizi ndizo picha ya filamu mpya ya Snake Kingdom ya Steve Nyerere ambayo inaandaliwa na kampuni ya Nyerere the Power. Katika filamu hii yenye uwondo wa kipekee, Steve ameigiza kama nyoka ambaye analeta kasheshe kubwa kwenye familia, na ndipo anaingilia hadi Familia ya mfalme huyo
 Wakari wengi wametikisa kwenye filamu hii, akiwemo Chuchu Hansi, Cath Lupia na wengine wengi, Chini ya uongozi wake Jacob Stephan 'Jb'